Kamati ya Maadili, Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF itakutana ili kujadili suala la usajili wa Ramadhan Chombo Redondo ambaye Azam FC wanadai bado ni mchezaji wao halali. Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema suala la Redondo litatolewa ufafanuzi leo Agosti 10.