HII NDIYO HARUSI YA WAZIRI MKUU WA ZIMBABWE KATIKA PICHA.
Posted on
Sep 17, 2012
|
No Comments
Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amefunga ndoa siku ya Jumamosi licha ya hukumu ya mahakama kutoa hukumu ya inayozuia ndoa hiyo kufanyika.
Siku ya Ijumaa mahakama ilifutilia mbali leseni ya ndoa ya Bwana Tsvangirai ikisema kuwa tayari anatambulika kuwa ameoa mwanamke mwingine katika sheria za kimila.
Mwandishi wa BBC nchini Zimbabwe anasema kuwa baadhi ya wafuasi wa Bwana Tsvangirai wanaamini kuwa hukumu hiyo ya mahakama imepikwa kisiasa ili kumchafulia jina Waziri mkuu huyo kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao.



