TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LARINDIMA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA USIKU HUU
Posted on
Sep 15, 2012
|
No Comments

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akitangaza namba ya mshindi wa bahati nasibu ya gari aina ya Toyota Virtz aliyejishindia gari hilo katika droo ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mkoani Dodoma kwenye tamasha la lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku huu, aliyeshika kompyuta ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile Rugambo Rodney, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Lephy Gembe na wa pili kutoka kulia ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Humud.
Katika tamasha hilo wasanii mbalimbali wanatumbuiza katika tamasha hilo kubwa baada ya matamasha mengine kama hayo katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida na sasa leo mkoani Dodoma.

Waigizaji wa filamu wakielezea uwezo wao katika kusakata muziki kutopka kulia ni Jacob Steven JB, Wema Sepetu, na Aunt Ezekikel.





Shetah msanii wa muziki wa kizazi kipya bongofleva akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,








