NCHI ZA MAGHARIBI ZATOA WITO WA KUSITISHWA KWA MASHAMBULIZI KATIKA BALOZI ZAO.
Posted on
Sep 15, 2012
|
No Comments

Nchi za magharibi zimetoa wito wa kusitishwa na kumalizika kwa maandamano na vurugu zinazoendelea zinazolenga balozi za nchi zao, zinazochochewa na kuonyeshwa kwa filamu inayodaiwa kumkashfu Mtume Muhammad.
Umoja wa Ulaya umewataka viongozi katika nchi za Kiarabu na Kiislamu kutoa wito wa amani.
Marekani imechukua hatua ya kupeleka manowari za kivita kulinda balozi zake katika mji wa Khartoum na kutoa wito kwa Mamlaka ya Sudan kutoa ulinzi kwa wanadiplomasia wa kigeni nchini humo.
Takriban watu saba wamekufa katika maandamano miji ya Khartoum Tuni na Cairo.