TASWIR ZA SHUGHULI MBALIMBALI ALIZOFANYA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE ZIARA RASMI NCHINI KENYA
Posted on
Sep 15, 2012
|
No Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipanda miti wakati walipozuru mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke utokao chini ya ardhi wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mwenyeji wao Rais Mwai E. Kibaki Wakisaini kitabu maalum baada ya kuwasili nchini Kenya, Jumanne, 11 Septemba , 2012, kuanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.


Baadhi ya mawaziri na maofisa waliondamana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Kenya

Baadhi ya mawaziri na maofisa waliondamana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Kenya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wake wa Chuo Kikuu cha Kenyatta baada ya kufungua Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.Picha na IKULU