DK. HARRISON MWAKYEMBE APOKEA TAARIFA YA KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA UTENDAJI KAZI WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA).
Posted on
Oct 21, 2012
|
No Comments

Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya kutoka kwa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Bw Bernard Mbakileki Wizarani Leo. Kamati hiyo
ya watu wanane iliundwa tarehe 27 Agosti 2012 kwa ajili ya kuchunguza
utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA).Waziri wa Uchukuzi ameiahidi Kamati kuwa kila kipengele
walichoshauri kwenye ripoti hiyo kitachukuliwa hatua na Mpaka Disemba
mwaka huu Utekelezaji wa Mapendekezo ya ripoti yatakuwa yametekelezwa
yote.

Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Bernard Mbakileki akionyesha
Magazeti mbalimbali kwa Waziri wa Uchukuzi,Watendaji wa taasisi za
Wizara Uchukuzi pamoja na waandishi wa habari hawapo pichani yaliyokuwa
yakiripoti mambo mbalimbali wakati uchunguzi huo ulipokuwa ukiendelea.

Mwenyekiti wa kamati ya ya uchunguzi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania(TPA), Bw Bernard Mbakileki akisistiza jambo kwa Uongozi wa
Wizara ya Uchukuzi,Taasisi zilizo chini ya Wizara na waandishi wa
Habari(hawapo Pichani),wakati wa kukabidhi ripoti waliyoiandika kwa
Waziri wa Uchukuzi na kuikabidhi leo. Kulia kwa Mweyekiti wa Kamati hiyo
ni Mhe. Mhandisi. Ramo M. Makani.(Mb) ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo.

Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa
Habari(hawapo Pichani)baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya watu wanane
aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania(TPA).Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa mapendekezo
yalioandikwa kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi na kila aliyehusika na
ubadhilifu atachukuliwa hatua.

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea ripoti ya Kamati iliyoundwa Kuchunguza Utendaji kazi wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Benard
Mbakileki,Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Naibu Waziri wa Wizara ya
Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, na Kushoto kwa Naibu Waziri huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo.
