VIONGOZI SITA WA UAMSHO WATIWA MBARONI.
Posted on
Oct 21, 2012
|
No Comments

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu 65 wakiwemo viongozi sita wa kundi la Uamsho na Jumuiya ya Maimam Zanzibar kwa tuhuma za kuchochea ghasia na vurugu zilizosababisha vitendo vya uporaji wa mali na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insptekta Mohammed Mhina,
amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa viongozi hao wa Jumuia mbili za
Kidini mjini Zanzibar, Polisi pia imewakamata watu wengine sita kwa
tuhuma za mauaji ya Askari Polisi.
Insepekta Mhina, amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimau
Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmed(41) mkazi wa Mbuyuni na Sheikhe
Mselem Ali Mselem(52) wa Kwamtipura ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar.
Wengine
ni Sheikhe Azan Khalid Hamadi(48) wa Mtendeni, Hassan Bakari
Suleiman(39) wa Tomondo na Ustaadh Mussa Juma Issa(33), Suleiman Juma
Suleimain(66) pamoja na Mussa Juma Issa(37) wote wa Makadara mjini
Zanzibar.
Inspekta Mhina amesema viongozi waliokamatwa ni wale walikuwa wakihojiwa na Polisi tangu jana kwa lengo la kutafuta ukweli wa taarifa za kutekwa kwa Sheikhe Farid Hadi Ahmed kulikopelekea ghasia na uharibifu mbalimbali kabla ya kujitokeza tena hadharani juzi.
Akizungumza
na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kamamishina wa Polisi Zanzibar CP
Mussa Ali Mussa amesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo linaendelea
na operesheni maalumu ya kuhakikisha kuwa kila aliyehusika katika ghasi hizo anakamatwa na kukabili mkono wa sheria.
Akizungumzia maendeleo ya Upelelezi wa Kesi ya Kuuawa
kwa Askari Polisi CPL Said Abdarahaman Juma aliyeuawa usiku wa kuamkia
Alhamis wiki iliyopita, Kamishna Mussa amesema Polisi wamefanikiwa
kuwatia nguvuni watu sita kwa kuhusika na mauaji ya askari huyo.
Amesema hadi sasa Polisi inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya askari huyo ambapo watuhumiwa watatu walikamatwa mjini Zanzibar na wengine watatu wamekamatwa mkoani Tanga.
Kamishna Mussa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Mohammed Said(35) wa Mwanyanya,
Joli Gasuli(20) wa Vuga, Bakari Juma Yusufu(22) wa Mwembe Makumbi na
Amour Rished(40) wa Bububu ambao walikamatwa mjini zanzibar siku ya kwanza lilipotokea tukio hilo.
Amewataja watuhumiwa wengine ambao wamekamatiwa Mkoani tanga na ambao tayari
wamesharejeshwa Zanzibar kuwa ni Ali salum Seif(21) na Abubakari Haji
Mbarouk(32) pamoja na mdogo wake Mohammed Haji Mbarouk(21) wote wakazi
wa Ndagaa mkoa wa Kusini Unguja.
Kamishna Mussa amesema Polisi bado inaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na wale watakaobainika kuhusika na mauaji ya askari huyo watafikishwa mahakamani.
Amesema kwa ujumla tangu kukamatwa kwa viongozi hao hali ya usalama katika mji wa Zanzibar imerejea upya na wananchi wameombwa kutoshabikia vitendo vyovyote vile vitakavyoweza kupelekea uvynjifu wa amani.
Amewataka
Wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kshiriki katika mikusanyiko na
kuwa chanzo cha fujo na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo
atashughulikiwa ipasavyo na mkono wa dola.
