HIVI UMEISIKIA KAULI YA DR ULIMBOKA? SENTENSI ZAKE NNE PAMOJA NA ALIEMTAJA VIKO HAPA.
Posted on
Oct 18, 2012
|
No Comments

Baada ya kukaa kimya kwa muda
mrefu toka arudi Tanzania kutoka kwenye matibabu, hatimae mwenyekiti wa
Jumuiya ya madaktari Dr. Steven Ulimboka ameamua kuweka wazi jina la mtu
aliempigia simu na kukutana nae muda mfupi kabla ya kutekwa na kuteswa
na kisha kutelekezwa kwenye msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Dar es
salaam usiku wa july26 2012.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyoandaliwa na Dr. Ulimboka na kusainiwa na mwanasheria wake
Rugemeleza Shayo ambayo imesomwa kwa vyombo vya habari na wakili wake
Nyaronyo Kichele, imeeleza kwamba siku aliyotekwa na kuteswa alikua na
mawasiliano na afisa usalama aliemtaja kwa jina la RAMADHANI ABEID
IGUNDU na kuamplfy zaidi kwamba anashangaa mpaka sasa huyu mtu
hajakamatwa wala kuhojiwa.

Dr Ulimboka hospitalini june 29 2012.
Kwenye hiyo taarifa, pia Dr.
Ulimboka amesema taarifa zote zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari
kuhusu yeye ni za kweli ambapo amesema yuko tayari kuweka wazi ukweli
wote iwapo itaundwa tume huru kushughulikia jambo hilo ili haki
itendeke.
Namkariri kwenye taarifa yake
akisema “Mimi Ulimboka Steven ni raia wa Tanzania ambae ninafahamu nina
haki ya kuishi na kuwa serikali yangu na wananchi wenzangu wanajukumu la
kuulinda uhai wangu, wale wote waliotuhumiwa na ninaowatuhumu
kunitendea unyama huu wako huru na hakuna aliewagusa, je uhai na maisha
yangu yana thamani ndogo kama ya mnyama anaekwenda machinjioni?”- Dr.
Ulimboka
Kwenye sentensi ya mwisho
namkariri Dr Ulimboka akisema “Je serikali ya nchi yangu itakubali lini
kuundwa kwa tume huru kuchunguza unyama huu na kuhakikisha kuwa haki
inatendeka? je kuna watu katika nchi yetu ambao wana haki ya kutenda
unyama kwakuwa wako juu ya sheria? hiyo sio Tanzania ninayoifahamu, niko
tayari kuhojiwa na kutoa ushirikiano wangu kwa vyombo huru na makini
vya uchunguzi ambavyo vitaundwa kuubaini ukweli”