photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > KIONGOZI WA KUNDI LA UAMSHO SHEIKH FARID NA BAADHI YA WAFUASI WAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO.

KIONGOZI WA KUNDI LA UAMSHO SHEIKH FARID NA BAADHI YA WAFUASI WAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO.

Posted on Oct 22, 2012 | No Comments

Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.
Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.
Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi.
Gari la Polisi ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linawasili Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.Viongozi hao wote walirudishwa rumande.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).


Toa Maoni Yako Kwa Uhuru