MAJADILIANO YA KUISAIDIA TANZANIA KIUCHUMI YAENDELEA JAPAN.
Posted on
Oct 12, 2012
|
No Comments

Ujumbe
kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa
pamoja na maafisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu
ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kuendelea
kiuchumi hapa Jijini Tokyo- Japan.

Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. William Mgimwa akiwa na ujumbe katika mkutano, wa
kwanza kulia ni Bi. Salome Sijaona ambaye ni Balozi nchini Japan
akifuatiwa na Bw. Siyvacius B. Likwelile Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha akifuatiwa na Bw. Khamisi Mussa Omari Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha Zanzibar katika mkutano Jijini Tokyo- Japan.

Wa pili kutoka kulia ni
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar
Diop,akiwa ameambatana na Maafisa Waandamizi kutoka Benki ya Dunia
wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa hayupo
kwenye picha.

Wa
kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan Bi. Salome Sijaona
akifuatiwa na Dk. Servacius B. Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha akifuatiwa na ni Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa
na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omari walioko
nyuma ni maafisa waandamizi wa Tanzania Jijini Tokyo – Japan
wakimsikiliza kwa makini Bw. Makhtar Diop, ambaye ni Makamu wa Rais wa
Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika.

Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop,akiwa
ameambatana na Maafisa Waandamizi kutoka Benki ya Dunia wakati wa
mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa ambaye yuko na ujumbe
wake kutka Tanzania pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Japan Bi.
Salome Sijaona katika kikao cha pamoja cha ambacho Mheshimiwa Waziri
alikutana na Kiongozi huyo kwa madhumuni yakutoa mapendekezo ya maeneo
ambayo Tanzania tukisaidiwa tutasonga mbele kiuchumi.

Kushoto
kwa Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ni Maafisa kwa Benki ya Dunia
wakifuatilia kwa makini kuhusu mkutano huo wakiwa pamoja na ujumbe
kutoka Tanzania hapa Jijini Tokyo – Japan.

Waziri wa fedha Mhe. Mgimwa akifafanua jambo kwa Afisa wa Benki ya Dunia.

Gavana
wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu akitoa maoni yake kwenye mkutano na
Makamu wa Rais wa Dunia hayupo pichani hapa Jijini Tokyo- Japan.

Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop
akifurahia jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe.
William Mgimwa hayupo kwenye picha.
