OBAMA AMFUNIKA ROMNEY KWENYE MDAHALO WA PILI, TAZAMA VIDEO YA MDAHALO HUO
Posted on
Oct 17, 2012
|
No Comments

Baada ya kuonekana alishindwa kummudu Mitt
Romney kwenye mdahalo wa kwanza sasa Barack Obama amerejea na nguvu mpya katika
mdahalo wa pili na kumfunika Romney.
Ikiwa ni muendelezo wa midahalo mitatu
iliyopangwa kufanyika kati ya Obama wa Democratic na Romney wa Republican watu
wanaomsapoti Obama alfajiri hii walikuwa na kila sababu ya kutabasamu pale
ambapo Obama alionekana kummudu mpinzani wake katika mdahalo huu wa pili.
Kwa mujibu wa kura zilizopigwa kupitia CNN
Obama amepata asilimia 46 dhidi na Romney ambae amepata asilimia 39.
Obama aliweza kumbana Romney na kama
alivyosema kuhusu mdahalo wa kwanza kuwa Romney anapoint nzuri lakini haziwezi
kufanya kazi kwa masikini na matajiri, katika mdahalo huu pia imeonekana hivyo
kuwa haziwezi kufanya kazi katika U.S.A yenye mchanganyiko wa masikini na
tajiri bali zitawafaidisha matajiri zaidi.
Wakati wa mdahalo huo watu mbalimbali
ulimwenguni kote walikuwa wanatweet kuhusu mdahalo huo na inaonekana zaidi ya
tweet million 7 ziliandikwa.
Bado mdahalo mmoja tu uliobaki ili
kuwapisha wananchi wa U.S.A kuchagua nani aingie White house na sasa Obama
amesawazisha bonde alilokuwa ameweka wakati wa mdahalo wa kwanza na inaweza
kuwa ameteka kura mpya kadhaa kurudisha wale aliokuwa amewapoteza baada ya
mdahalo wa pili.
Itazame debate nzima hapa....