AKAMATWA UWANJA WA NDEGE AFRIKA KUSINI AKIWA NA VIPANDE 220 VYA ALMASI TUMBONI.
Posted on
Nov 15, 2012
|
No Comments

Jamaa
mmoja mwenye asili ya Lebanon amekamatwa nchini Afrika Kusini wakati
akisubiri kupanda ndege katika kiwanja cha ndege cha jijini Johannesburg
kuelekea Dubai.
Polisi
nchini Afrika Kusini wamesema jamaa huyo alikuwa amemeza vipande 220
vya almasi kwa nia ya kuvisafirisha nje ya nchi hiyo.
Maafisa
hao wamesema kipimo cha picha ya mwili wake kilionyesha vipande hivyo
vya almasi vyenye thamani ya Dola za Marekani milioni 2.3, sawa na
paundi milioni milioni 1.4 za Uingereza au Euro milioni 1.8 za Umoja wa
Ulaya ambazo ni takribani zaidi ya shilingi milioni 355 za Tanzania.