Wakati mwingine najilaumu, 'kwa nini nimesikia?' 'kwa nini nimeona?'
Nataka nizungumzie kauli ya Mh. E. LOWASA.
Katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa huko Manyara, huyu baba kasema hivi!
"Katika ilani ya ccm 2015 elimu ya sekondari iwe bure! Serikali ina
'FEDHA NYINGI' zinazotumika kujenga barabara na shughuli nyingine.., na
elimu hii iwe na quality, mwanafunzi akimaliza awe anajua kila kitu..."
Akili kumkichwa,
-kwa nin 2015?
-amegundua lini kuwa serikali ina 'fedha nyingi?
-kwa nin Chadema waliposema inawezekana wao walisema HAIWEZEKANI?
-anamwagiza nani abadili ilani ya Ccm kule kanisani?
-anazungumzia fedha zipi ambazo miaka yote aliyopo uongozini hazikuwepo?
Najuta kuwaza!
Wake up!
Natafuta wa kunipiga kibao nihakikishe kama nipo usingizini au la! Najipa moyo kuwa hii ni ndoto tu.