UCHAGUZI WA AMANI UMEWEZEKANA SIERRA LEONE.
Posted on
Nov 18, 2012
|
No Comments

Wasimamizi
wa uchaguzi nchiniSierra Leonewamesema uchaguzi mkuu nchini humo
umefanyika kwa amani na uwazi na kwamba watu wengi walijitokeza jana
kupiga kura, ingawa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilichelewa
kufunguliwa.
Hamid
Goutierez, msemaji wa kituo cha waangalizi cha Carter, amesema katika
suala la taratibu kwa ujumla wamebaini ni mchakato unaoaminika. Mkuu wa
ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Richard Howitt amesema wananchi
wengi wa Sierra Leone wamesema uchaguzi wa mafanikio utakuwa ishara ya
nchi hiyo kusonga mbele kutoka kwenye taifa linalojitoa kutoka mzozo
wa vita na kuwa taifa la maendeleo.
Huu
ni uchaguzi wa tatu kufanyika tanguSierra Leoneitoke kwenye vita vya
wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002, ambapo watu 50,000 waliuawa. Rais
aliyeko madarakani, Ernest Koroma na chama chake tawala cha All People’s
Congress anapambana na Julius Maada Bio, kiongozi wa zamani wa kijeshi.
Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa ndani ya siku kumi.