MAELFU WAFURIKA KIBANDAMAITI KUPONGEZA SAFU MPYA YA UONGOZI WA CCM.
Posted on
Nov 18, 2012
|
No Comments

Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
akiingia uwanjani wa Kibandamaiti, Wilaya ya Mjini, wakati wa sherehe za
Wana-CCM Zanzibar kuipongeza safu mpya ya uongozi. Kulia ni Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana na Watatu Naibu Katibu Mkuu (Bara) Vuai Ali
Vuai.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia Uwanja wa Kibanadamaiti katika
sherehe ya wana-CCM wa Zanzibar kupongeza safu mpya ya uongozi wa CCM
Taifa. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu
Mkuu (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye.

Mamia
ya wana-CCM Uwanja wa Kibandamaiti, wakati wa sherehe za wana-CCM wa
Zanzibar kuipongeza safu mpya ya uongozi wa CCM Taifa.

Makatibu
wa NEC, Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni) na Asha-Rose Migiro (Siasa
na Mambo ya Nje) wakiteta jambo wakati wa mkutano wa wana-CCM Zanzibar
kuipongeza safu mpya ya uongozi wa CCM Taifa, kwenye viwanja vya
Kibandamaiti, mkoa wa mjini.

Vijana wa CCM wakishangilia kwa mtindo wa aina yake wakati wa sherehe hizo (Picha zote na Bashir Nkoromo).

Wakiserebuka.

Makamu
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni akihutubia mamia ya
Wana-CCM Kwenye Viwanja Vya Kibanda Maiti, Mkoa Wa Mjini, Mjini
Zanzibar katika Sherehe ya Wana-CCM Zanzibar kupongeza Safu mpya ya
Uongozi wa CCM Taifa. (Picha Na Bashir Nkoromo).