UK YAIKATIA UGANDA MISAADA KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Posted on
Nov 18, 2012
|
No Comments
Waziri wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Justine Greening amesema serikali ya
London imesitisha misaada ya takribani dola milioni 18 kwa serikali ya Uganda
kutokana na kuwepo tuhuma za ufisadi katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Greening amesema misaada hiyo haitatolewa hadi pale Kampala itakapochunguza tuhuma hizo na kuchukua hatua zifaazo.
Waziri huyo amesema fedha hizo zinatokana na ushuru wa wananchi wa Uingereza na kwa mantiki hiyo wanataka kuona fedha zao zikitumika kuwasaidia wale wanaohitaji misaada ya dharura.
Katibu wa kudumu katika ofisi ya Waziri Mkuu nchini Uganda anatuhumiwa kufuja fedha za umma hususan zinazotokana na misaada ya kigeni lakini kiongozi huyo amekanusha tuhuma hizo sambamba na kukataa kujiuzulu.
Ikulu ya Rais mjini Kampala pia imeonekana kumkingia kifua katibu huyo kwani imesema haiwezi kumuachisha kazi iwapo hakuna ushahidi unaoonyesha ameiba mali ya umma