MLIPUKO ULIOUA WATU 7 KENYA WASABABISHA TAFRANI, WASOMALI WAPIGWA POLISI WAFYATUA RISASI.
Posted on
Nov 19, 2012
|
No Comments

Abiria
wasiopungua 7 waliuwawa jana na wengine zaidi ya 33 kujeruhiwa wakati
dalala ‘matatu’ iliyokuwa njiani kuelekea Kariobangi ikitokea jijini
Nairobi iliposhambuliwa kwa bomu katika kitongoji cha Eastleigh, katika
mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Mkuu
wa jeshi la polisi katika mkoa wa Nairobi, Moses Ombati, amesema
walioshuhudia tukio hilo walimuona mtu akishuka kutoka kwenye matatu
hiyo na kujaribu kuingia matatu nyingie iliyokuwa nyuma lakini akaanguka
na kushambuliwa na umma. Ombati amesema hawana hakika kama mtu huyo
alihusika na shambulizi hilo lakini wanafanya uchunguzi wa kina.
Dakika
chache baadae vijana waliokuwa na hasira waliwalenga watu wa jamii ya
Kisomali kwenye mtaa huo, Polisi ilibidi kufyatua risasi hewani
kuwatawanya watu.