BASI LA SAI BABA KUACHA NJIA , KUINGIA VICHAKANI, WATU WATANO WAJERUHIWA.
Posted on
Mar 31, 2013
|
No Comments
Abiria wapato 45 waliokuwa wakisariri na basi la Sai baba kutoka mjini Dar es salam kuelekea Masasi mkoani Mtwara wamenusurika kufa kutokana na gari yao kuacha njia na kutumbukia vichakani.
Waliojeruhiwa ni dereva, kondacta wote wakazi wa jijini Dar es salaam na abiria wengine watatu.
Said Mkubwa ambaye ni kondacta wa gari hilo alisema ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka tairi la mbele upande wa kulia wa dereva ambapo gari liliacha njia na kutumbukia mtoni chini ya daraja la Mbanja.
Majeruhi wote watano wamefikishwa hospitali kwa matibabu zaidi.
