Ah!, Bi Kidude tulikuwa naye jamani katika safari yetu kama mnavyoona akipozi kwa picha na wafanyakazi wa unwaja wa ndege wa Moroni
|
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara kampuni ya ndege ya ATC Mwanamvua Ngucho akihojiwa na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kiamtaiafa wa Prince Said Ibrahim Ahaya Njini Moroni Comoro mara baada ya ndege ya shirila hilo kuwasili katika uwan ja huo, Shirika la ndege la ATC limeanzisha safari za Dar es salaam Comoro leo, katika picha kulia ni Sitti Mohamed Nourou.mwakilishi wa kampuni ya ATC Nchini Comoro kutoka Shirika la Com Air |
|
Wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya ATC wakitoa huduma kwa abiria wakati wa safari ya ndege hiyo kutoka Dar es salaam kwenda Moroni visiwa vya Comoro. |
|
Wadau kutoka kampuni ya Push Mobale tuliambatana nao na ilikuwa burudani kweli. |
|
Mmoja wa wafanyakazi wa ndege ya shirika la ndege la ATC akitoa maelekezo ya vifaa vya usalama kwa abiria wa ndege hiyo |
|
Moja ya eneo la mji wa Moroni visiwa vya Comoro linavyoonekana angani. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara kampuni ya ndege ya ATC wanamvua Nguchu akisalimiana na maafisa usalama wa uwanja wa ndege wa Prince Said Ibrahim Ahaya mjini Moroni mara baada ya ndege hiyo kuwasili nchini humo. Source; Fullshangwe Blog | |
|