photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > PICHA NA HABARI KAMILI ZA MLIPUKO WA BOM ARUSHA.

PICHA NA HABARI KAMILI ZA MLIPUKO WA BOM ARUSHA.

Posted on May 5, 2013 | 27 Comments


Watanzania wenzangu,













Kwanza niwape pole kwa yaliyotokea Arusha asubuhi hii, hili ni tukio la kusikitisha na linalostahili kulaaniwa na kila mpenda haki na muumini wa uhai duniani bila kujali dini yake.


Kwa haraka haraka napeleka lawama zangu kwa waislamu wenye msimamo mkali. Lakini naomba nieleweke na mnielewe, hili ni kundi dogo tu la waislam na si sawa wala haki kuwalaumu waislamu wote hata itakapobainika ni waislamu wenye msimamo mkali ndio wamehusika.

Watanzania wenzangu tukumbuke kwamba kabla ya kuwa waislamu, kabla ya kuwa wakristu, tulikuwa wapare, wamakua, wahaya, wasukuma nk. Dini zimekuja juzi tu na si sawa zitutenganishe na kutugombanisha.

Sasa kuliko kipindi chochote tunahitaji umoja kama watanzania, tusianze kunyoosheana vidole kwa misingi ya dini, tuelewe kuwa hili ni kundi dogo la watu wasiowakilisha watu wote wa dini hiyo.

Mwisho ni jukumu la serekali kutuhakikishia usalama wetu kama Watanzania. Ni wazi kuwa vyombo vyetu vya usalama havina uwezo wa kuchunguza na kupata ukweli kuhusu shambulio hili, tunataka vyombo vya nje vyenye uweledi katika uchunguzi wa matukio ya kigaidi kama haya vihusishwe tujue ukweli kuhusu tukio hili.

Namaliza na rai yangu, NOW MORE THAN EVER WE NEED TO STAND TOGETHER AS TANZANIANS!
From; Jamiiforum. 

Comments: 27

  1. asanteeeee.
    ts really depressing how far this few muslims are willing to go for somethings that do not make sense.

    ReplyDelete
  2. Maisha ya watanzania sasa ni kama ya ndege anayeishi juu ya mti. usalama wa taifa na wapelelezi wamebaki kutafuta mbinu za kudhoofisha chadema lakini wamesahau kutoa majibu kwa matukio ya kigaidi yanayotikisa hasa kundi la wakristu hasa wakatoliki. hakuna umakini(seriousness) unaojidhihirisha kwa matokeo ya kigaidi yaliyotokea mauaji ya padre na kupigwa risasi padre kule zanziba. wala hakuna majibu kwa waliochoma makanisa zanziba, dar na kigoma.

    lakini cha kushangaza kila inapofika serikali ina tuhuma za kujibu kwa wananchi mfano tuhuma juu ya elimu na ufisadi unaotakiwa kupatiwa majibu ndipo matukio ya kufadhaisha yanajitokeza ili kuwasahaulisha watanzania masuala nyeti kama haya ya hujuma ya katiba mpya.

    sasa watanzania tusali. tuombe amani. tushikamane tuwe wamoja. tuchambue matukio haya kwa amani.
    tuchukue hatua ya kuwafahamu maadui zetu ni kina nani. tukishawajua tuchukue hatua kwa pamoja. harufu ya mashambulizi haya ilishaenea mitaani hasa mitaa ya arusha kwenye parokia iliyokumbwa na madhila haya. lakini usalama haukuchukulia hatari kama ugaidi. lwakatare ndiye gaidi bila shaka. ambaye ni kitisho kuliko hatari ya leo. ulimboka na kibanda pia hawakukumbwa na ugaidi. bali waliowatesa walisifiwa na baadhi sauti zilizosikika bungeni zilisema ''amezidi" wakati mnyika analeta hoja bungeni kuhusu kauli iliyotolewa na pinda na tukio la kuhujumiwa uhai kwa ulimboka. mwangosi hakufanyiwa ugaidi bali ni bahati mbaya.

    ee Mungu wewe unakaa mahali pa juu sana ambapo mwanadamu hawezi kupafikia kwa sababu ya utukufu wako. fanya miujiza ya kuwaweka watanzania masikini mikononi mwako na uwaepushe wa madalali wa uhai wetu ambao wengine wana mamlaka na nguvu ya kutufanyia watakacho. AMINA.

    ReplyDelete
  3. ........Mimi haya siyashangai hata kwenye Taasisi za umma watu tumekuwa tukinyanyaswa sana na watu hao wenye madaraka ya Nchi na ofisi kwa jumla, kimsingi serikali hii iliyopo madarakani haiwezi kukataa kama haya si mavuno ya mbegu iliyopandwa na wao na chama chao.....

    ReplyDelete
  4. Hope there is a figure up thr in the gvt inayojihusisha na unyama huu,Mungu wetu sio binadam na hakika machoz yetu yatalipwa tu,,,serikali haiwez kushindwa kujua whatz happening,imeamua iwe hiv ili mambo flan yatimie,,,,,Inauma sana

    ReplyDelete
  5. maneno ya mkosaji wewe mwenye hii forum unaonekana ni mtu limbukeni kwani hata huna ushahidi unakaa kazi ya kuleta chuki dhidi ya uislam. unaushahidi wa hili kusema ni waislam wamehusika au kwasababu una kinywa kipana???????????????

    ReplyDelete
    Replies
    1. we acha hizo kwani kasema waislamu wote soma vizuri kabla hujaongea, na hata hivyo dalili inaonesha badhi ya waislamu wanahusika unakata nini wewe acha hizo sometime lazima unakubali matokeo sio unagoma tu. Ndio nyie mkiletewa kesi za watoto wenu kuwa wezi unakataa kabisa mpk uletewe maiti ya mwanao...

      Delete
  6. NANI KATANGAZA KUWA NI WAISLAMU WAMEFANYA HIVYO ?

    ReplyDelete
  7. msitoe majawabu kwenye kitu ambachohamkijui.jekama niM23 je? si ndowamerudisha majibu yaoya bungeni na mbwembwe za Waziri wa Mambo Ya jana. tuwe waangalifu watanzania hii ni nchi yetu.

    ReplyDelete
  8. Mwandishi aliyechambua hapo mwanzo/juu perhaps ni mwenye blog or whatever ameandika kwa mtitiririko nzuri wenye mantiki ya ustaarabu yenye kulenga amani na maridhiano. Nimeshangaa kuona huyo ..anonymous aliye sema 'maneno ya mkosaji'....nk. kutoa shutuma za kumshambulia muhusika(direct attack). Mbona unajishtukia?
    Hapa sasa dunia nzima inaweza kujionea jinsi ile roho ya uasi inayoleta kansa duniani inavyosambaza sumu zake. Vurugu za maeneo mbalimbali ya duniani hapa ni kutokana na roho hiyo.

    Tuheshimu uhuru wa mtu kutoa mtazamo au maoni yake maana ni haki yake kikatiba maadam haivunji katiba na si kumshambulia mtu.
    POLENI WAHANGA WOTE WA USHETANI HUO ULIOFANYIKA HUKO ARUSHA POLENI PIA WAPENDA AMANI WOTE DUNIANI. UKWELI, HAKI NA AMANI NDIYO SILAHA KUBWA KULIKO HAYO MABOMU YAO. I PRAY FOR YOU ALL NOW AND ON.

    ReplyDelete
  9. Ninyi watanzania kuweni makini,haya tuliyaona Rwanda na Burundi, yatakuja hata hapa, sijui wahusika ila itafika mahali tutachoka baada ya kubaini ukweli na tutasemaaaa, enough is enough, japo nawaasa muwe makini na kuwachagua viongozi kataka ngazi zote, chagueni watu wenye weledi, wasio wanafiki,nchi hii imekuwa nchi ya fitna, chuki, maasi mbali mbali yote haya chanzo chake ni siasa chafu zilizojaa fitna na chuki kama ilivyo kwenye chama cha mpira,ukweli utafichuka na wote tutaujua japo yapo mambo fulani fulani ambayo yapo wazi.....endeleeni, nyie wahusika hakika mtavuna mnacho kipanda

    ReplyDelete
  10. Huwezi kuyatengenisha na uislamu pamoja na serikali,kwani serikali imekua inawalinda hatuoni usalama wa taifa ikifanyia kazi matukio kama haya na kuwafunga au kuwanyonga wahusika, lakini wakumbuke Mungu anasimamia haki, wanaofanya uovu huu watafika mpaka huko kwenye office za serekali na hawatajali ni nani yuko ndani ya office, na watawadhuru. ukifuga nyoka iko siku itakug'ata, kwa kua serekali inawalea iko siku watawarudi

    ReplyDelete
  11. Mungu wetu ni mwema. Na siku zote usimama katika haki. Ninaami tukimkimbilia yeye hatutahaibika. Najua leo wanajiona wajanja kwa yaliyotokea lakini iko siku mungu atasimama na ataonyesha ukuu wake. Nawasii wezangu tuzidi kiomba amani na upendo ktk nchi yetu.

    ReplyDelete
  12. Yote yana mwisho kwani Mungu ni mkubwa kuliko ibilisi yoyote na matendo yake kupitia watu, Watanzania tushikamane, tusimpe adui nafasi, utafiti naufanyike na tusiloweza wala mwanadamu yeyote, tumwachie Muumba. Ataweka kila kitu wazi ktk muda mhafaka hata kama baadhi watasumbuka na kuteseka, machozi yao yatapanguswa. Amani na uhuru vidumu Tanzania, dini na zituunganishe na siyo kututenganisha.Ee MUNGU MJALIE HEKIMA KILA MTANZANIA NA MKAAJI WAKE, AMINA

    ReplyDelete
  13. TATIZO TANZANIA WANASEMA NI MCHI HURU ILA SIYO KWELI MAANA USALAMA WA TAIFA NI CHOMBO KIPO LAKINI HAKIPO HURU KUSEMA UKWELI HATA WAKISEMA WATASEMEA WAPI MAANA WALIPO MADARAKANI NI HAO HAO NI TUSEME NI KAMA MAJASUSI MAANA WANAONA KINACHOENDELEA WANASEMA WATAUNDA TUME JE HIYO TUME NI NANI SI HAO HAO KWA HIYO HAKUNA HAKI YOYOTE NDIYO MAANA WATANZANIA WAMECHOKA WANYONGE TU NDIYO WATAKAMATWA NA KUFANYIWA WANAVYOTAKA NA KUENDESHA KESI ILA IPO SIKU WATAJIBU HIZI DAMU ZA WATANZANIA NA MUNGU PEKE YAKE NDIYO ATAKUWA MTETEZI WA WA TANZANIA MAANA HANA MTAZANIA ASEME NINI HAKUNA WALA HUSIKIKI KAMA HAUPO NGAZI ZA JUU TENA UWE UNAKUBALIANA NA MAAMUZI YAO, LAKINI KILA LENYE MWANZO IKO SIKU LUNAMWISHO WAKE.

    ReplyDelete
  14. Haya ndiyo matokeo ya Udini katika Tanzania!

    ReplyDelete
  15. Nitoe comment kidogo juu ya huyo aliyesema 'maneno ya mkosaji'maana inaonekana kama amejishtukia. Ni ukweli usiopingika kwamba waislamu wenye msimamo mkali "Muslim Fundamentalists" ndio wanaoleta matatizo makubwa duniani kote. Wanaleta matatizo hata kwa Waislamu wenzao! Jambo ambalo watanzania tunapaswa kuepuka ni misimamo ya kihafidhina ambayo dini yoyote ile inaweza kuwa nayo. Mathalan, wapo baadhi ya waamini ndani ya Ukristo ambao wanaamini juu ya VITA TAKATIFU au VITA YA MSALABA, wote hawa hawana tofauti na waislamu wenye msimamo mkali. Ukweli ni kuwa kama bomu linaweza kutupwa kanisani basi bomu hilohilo linaweza kutupwa msikitini, na mahali penginepo pa ibada, cha msingi tuangalie mambo ya kitaifa kwa kufikiria na kuchagua viongozi ambao wataimarisha umoja kitaifa badala ya hali ilivyo hivi sasa

    ReplyDelete
  16. HAYO NI MATOKEO AMBAYO WENYE AKILI TULIKUWA TUNATARAJI WAKATI WOWOTE YATATOKEA, NA SI TU KAMA YAMEISHA LA HASHA, YATAENDELEA KUTOKEA SASA WATANZANIA KAENI CHINI NA MTAFAKARI KWA KINA KWA NINI MAMBO HAYA YANATOKEA KIPINDI HIKI, UFISADI, GESI, UDINI, KATIBA? MTAHITAJI MSAADA ILI KUWEKA MAMBO YENU SAWA, SASA WATAKUJA WATOA MSAADA WAKUBWA DUNIANI (FREE MASSON) A.K.A USA KUWAPA MSAADA KWA MATATIZO YENU HATA MATATIZO YAKIPUNGUA GESI IMEKWISHA. TAFAKARINI WATANZANA........

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mhhh, hii nayo kali, lisemwalo lipo kama halipo laja, huenda kuna ukweli

      Delete
  17. Jamani hamjasoma kuwa aliyekamatwa amekiri kuwa yeye ni Muislam?

    ReplyDelete
  18. Chonde, chonde!!!
    hao lazima ni waislamu maana kuua kwao ni jambo la kawaida na wana assume kuwa ni thawabu ya kuwafikisha mbinguni. Ila ukweli ni kwamba lazima wataishia motoni hao tu na damu za watu zitawatafune popote waendako na mungu wa Islael fanya miujiza yako ili hao watambue kuwa wewe ndo muweza wa youte.

    Amen

    ReplyDelete
  19. Kukosekanan kwa msimamo dhabiti wa Rais na serikali yake dhidi ya vitendo hivi vyenye harufu ya udini ndiko kunakoleta haya yote,na bila msimamo huo kutokea hivi sasa, nchi itaparanganyika na watawala wa sasa kuingia kwenye historia ya kuiparanganyisha kwa misingi ya kidini(GORBACHEV wa TANZANIA).Rais Kikwete achukue ushauri wa mtangulizi wake BENJAMIN MKAPA kuwa wakati wake dini zilikua zikihubiri amani;aidha wakati wa Mwalimu NYERERE hatukuona mambo haya shauri ya misimamo yao dhabiti.Maneno matupu yasiyo na vitendo na utendaji yamekua kama motisha wa kimyakimya kwa hao wanaofanya vitendo hivyo kwani wanaona ni kama wana 'backing" ya kimyakimya ya viongozi wakuu na serikali.

    ReplyDelete
  20. Serikali ya Tanzania hamna kitu.
    Ngoja muda c mrefu watu wataanza chinjana kama kuku. Tuombe uzima maana ukikumbTI dogo ujue kubwa lake laja.

    ReplyDelete
  21. Pamoja na kumuomba Mungu katika kipindi hiki ambacho tunapitia magumu mengi watanzania tujifunze kufuatilia vitu ili kujua hatma yake ni nini, tuache tabia ya kumaliza mambo kimya kimya. kitu ambacho kimegusa jamii basi vyombo vya habari vipewe uhuru wa kupata taarifa kuhusiana natukio husika kisha kuijulisha jamii kwamba ni hatua gani zimechukuliwa bila kuleta siasa na urasimu. Ni haki ya kila mwananchi kujua nini kinafanyika katika nchi yake. Pia nashauri kesi za matukio kama haya zisichukue muda mrefu baada ya mtuhumiwa kukamatwa ili kupunguza mrundi kano wa matukio yanayo fanana kwani matukio haya yametokea mfululizo usio zidi miezi miwili miwili, mfano Makanisa ya Mbagala, Zanzibar na sasa Arusha na mengine mengi.

    ReplyDelete
  22. Hali ya nchi ni mbaya.

    Walishatangaza kuwa katika kipindi cha pasaka wanajiandaa kulipua makanisa. Kinachotokea kinaonekana kwa sasa. Na habari ndo hyo.

    Kwa nini watu hatufikirii maendeleo tunafikiria kuua watu tu?.

    ReplyDelete
  23. Ivi kwnza hyo s,,ch,, anajua maana ya ugaidi? ivo vijimlipuko vya bom makanisan ni tamaa za viongoz wa makanisa ssa leo hii makanisa yamekuwa kibiashara zaid wanatengeza michongo ya milipuko kuwalostisha kanisa flani na hii yote wakristo mnapenda misaada,,,,,,,,, muislam ata kwenye pango anaishi.

    ReplyDelete