photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > Dj, ManGi1; KASORO KATIKA VIDEO YA "SIHITAJI ,MARAFIKI NA MISS TANZANIA"

Dj, ManGi1; KASORO KATIKA VIDEO YA "SIHITAJI ,MARAFIKI NA MISS TANZANIA"

Posted on Jul 9, 2012 | No Comments

Evarist Chahali ni msomi aishiye Aberdeen,Scotland,nchini Uingereza ambako anasomea udaktrari wa Falsafa katika Siasa za Kimataifa,hususan kuhusu Afrika.
Pia anafanya utafiti kuhusu Uislam na Harakati za vikundi vya Kiislam nchini Tanzania. Alipata shahada ya Kwanza katika Elimu ya Jamii pale Mlimani (UDSM),kabla ya Kupata Shahada ya Uzamili katika Siasa na Uhusiano wa Kimataifa hapa Aberdeen,na baadaye Shahada ya Uzamili wa Utafiti (Master of Research-MRes) katika Utafiti wa Siasa (Political Research) huko huko Aberdeen.
Pamoja na kujihusisha na masuala siasa, hayuko nyuma katika kuusikiliza muziki wa kizazi kipya. Leo hii kupitia website yake ,www.chahali.com ameandika makala isemayo “Mapitio (Review) yasiyo rasmi ya video za SIHITAJI MARAFIKI (Fid-Q) na MISS TANZANIA (Solo Thang)”
Uchambuzi huu umetuvutia na tukaona si vibaya kama tukiuweka hapa pia japo sio wote.
Tumeuweka uchambuzi huu kwa kuanzia tu pale alipoanza kuzichambua video hizi na kama ungehitaji kusoma uchambuzi wote tembelea tovuti yake hapo juu.
“Sasa nageukia eneo linaloweza kuniingiza matatizoni: mapungufu katika kazi hizo za wasanii hao. Kimsingi si mapungufu bali ni pungufu kwani ni moja tu,na si kubwa sana.
Ukiangalia video zote mbili utabaini jambo hili: katika video ya Fid-Q,tangu mwanzo hadi mwisho wa video yake amevaa vazi lilelile.Kwa Solo,kwa kiwango kikubwa katika video hiyo yupo katika T-shirt ileile japo kuna vipande ambapo anaonekana amevaa shati.
Kama nilivyotanabaisha,hii ni kasoro ndogo inayoweza kabisa kufunikwa na ladha ( flavour) ya muziki, ujumbe uliomo katika wimbo,na kiwango cha video.Hata hivyo,kama inavyotanabaishwa kwenye na Andrew Goodwin kwenye Kanuni ya Video ya Muziki (Music Video Theory) vinavyoonekana katika video ya muziki (visuals) vinaweza kuwa na mchango mkubwa sio tu kuiboresha video husika bali pia kuiunganisha na hadhira.
Pengine ili uelewe ninachoelezea hapa nitolee mfano msanii kama Lady Gaga.Mavazi yake ni burudani tosha-japo sio aina ya mavazi unayoweza kumwambia fundi cherahani akutengenezee.Msanii kama Michael Jackson alifahamika sio tu kwa miziki yake bali pia mavazi yake.Kwa sanii wa hip-hop wa Marekani,mavazi ni moja ya vitu muhimu mno,na baadhi ya mapendezeo yao katika mavazi yamepelekea mwamko wa fasheni,kwa mfano mashati ya 'DOGI DOGI' yaliyokuwa yanapendelewa na wasanii wa rap/hiphop wa pwani ya magharibi ya Marekani (West Coast rappers) kwa mfano Snoop Dogg na Ice Cube.
Nadhani sababu pekee iliyowafanya Fid-Q na Solo wasionekane katika mavazi tofauti tofauti katika video zao ni MUDA.Hapa ninabashiri kuwa hawakuwa na muda wa kutosha kurekodi video zao kwa muda mrefu ambao ungewapa nafasi za kubadili mavazi mara kadhaa.
Naomba nisistize kuwa kasoro hiyo ndogo haijapoteza hata chembe ladha ya kazi zao bora kabisa.Nimeipigia mstari kasoro hii kwa minajili ya kuwasaidia wasanii hao huko mbeleni wajaribu kutumia muda zaidi katika kurekodi video zao.
Kanuni nyepesi ya kurekodi kitu chochote kile ni hii: kadri unavyojipa muda wa kutosha ndivyo unavyomudu kurekodi vitu vingi zaidi ambavyo wakati wa kuhariri utaondoa vile usivyovitaka na kuacha vile unavyovitaka.
Lakini kasoro hiyo ndogo inarekebishika.Ninaamini tulichoshuhudia katika video ya SIHITAJI MARAFIKI na MISSI TANZANIA ni matoleo ya mwanzo tu (iwapo Fid na Solo wana mtizamo kama wangu).Si ajabu kwa msanii kutoa video ya mwanzo kisha kutoa video nyingine rasmi kwa ajili ya wimbo husika.
Pengine kitawachowarahisishia Solo na Fid-Q kutengeneza video 'r(kama wataona kuna haja ya kufanya hivyo) ni ukweli kwamba tayari wana video nzima ya asili,ambapo wakiamua kuongeza chochote inakuwa ni suala la kuongeza tu vipande vipya katika original version.Hili si lazima,as long as wao wameridhika na versions walizoweka hadharani.
Ukiweka kando kasoro hiyo ndogo,Solo Thang ameendelea kuwa mithili ya balozi wetu wa Bongoflava katika anga za kimataifa ambapo anafanyia kazi zake kutoka nchini Ireland.Lakini licha ya kuwa nguli (legend) wa bongoflava na 'wadhifa' huo wa ubalozi wa kimataifa,msanii huyu ni miongoni mwa wachache ambao ni down-to-earth sana na anayejali sana kuishirikisha hadhira,hususan kupitia Twitter na Facebook.
Kadhalika,ana blogu yake anayotumia kuwafahamisha wapenzi wa muziki wake kuhusu kazi zake.
Kwa upande wa Fid-Q, mkongwe huyu wa muziki wa kufokafoka huko nyumbani amekuwa mahiri sana katika matumizi ya mitandao ya kijamii kutangaza kazi zake na kuishirikisha hadhira.Huko Twitter ana utaratibu wa kujibu maswali angalau mara moja kwa wiki kwa kutumia hashtag #AskFidQ. Hii inatoa fursa kwa wengi kumuuliza maswali mbalimbali.
Kadhalika,anaendesha kitu kinachofahamika kama Hip-Hop Darasa,ambapo pamoja na mambo mengine anatoa elimu kwa kizazi kipya cha Hip-hop huko nyumbani.Taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kipindi chake maarufu mtandaoni cha Fidstyle Friday kitaanza kuonyeshwa kwenye runinga katika kituo cha East Africa Television (EATV).Haya ni maendeleo makubwa.
Basi nimalizie kwa kuwapongeza Fid-Q na Solo Thang kwa kazi zao bora kabisa.Naomba wasitafsiri kasoro ndogo niliyobainisha hapo juu kuwa ni HATING. Sote tunapenda kuona wasanii wetu wakifanikiwa na kuteka anga sio huko nyumbani tu bali Afrika na duniani kwa ujumla.Natambua kuna wataosema "huyu nae,anajifanya anajua kila kitu" lakini lengo langu si kujifanya mjuaji bali kutoa mchango wangu kwa wasanii wetu.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru