photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> DR MIGIRO ATEULIWA KUWA MWAKILISHI MAALUMU UN AFRIKA SEKTA YA HIV-AIDS.

DR MIGIRO ATEULIWA KUWA MWAKILISHI MAALUMU UN AFRIKA SEKTA YA HIV-AIDS.

Posted on Jul 15, 2012 | No Comments

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemtetua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dr. Asha-Rose Migiro kuwa mwakilishi wake maalumu wa maswala ya HIV na UKIMWI barani Afrika.

Dr. Migiro atachukua nafasi ya Bi Elizabeth Mataka, ambaye amepongezwa na Bwana Ban kwa kazi yake nzuri tangu alipoteuliwa katika nafasi hiyo mwaka 2007. Dr.

Migiro anatarajiwa kutumia uzoefu na ufanisi wake katika kuendeleza juhudi za kukabiliana na UKIWMI kimataifa na katika bara la Afrika, wakati alipohudumu kama Naibu Katibu Mkuu tokea mwaka 2007 hadi 2012.

Wakati huo Migiro alikuwa mstari wa mbele katika kuchagiza mikakati ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya HIV miongoni mwa watoto wachanga ifikapo mwaka 2015, na kuunga mkono ujumbe wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon wa kukomesha ubaguzi na kuondoa unyanyapaa unaohusiana na HIV.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru