KATIBU MKUU WA CCM, WILSON MUKAMA AKUTANA NA MWEKEZAJI KUTOKA NIGERIA ALIKO DANGOTE WA DANGOTE INDUSTRIES LTD
Posted on
Jul 15, 2012
|
No Comments
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimkaribisha kwa bashasha, Mwekezaji kutoka Nigeria, Aliko Dangote, wa Dangote Industries Ltd alipowasili Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo, Julai 15, 2012, kwa ajili ya mazungumzo mbalimbali ikiwemo namna mwekezaji huyo anavyoweza kufanyakazi na Chama Cha Mapinduzi katika nyanja kadhaa za kibiashara. Katikati ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Nanjabu.
Mfanyabiashara wa Kampuni ya Dangote Industries Ltd ya Nigeria, Aliko Dangote akitia saini kitabu cha wageni Ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kulia) baada ya kiwasili. Kushoto ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Nanjabu.
Mukama na Ujumbe wa mgeni huyo wakiwa katika mazungumzo kwenye ukumbi wa sektretarieti Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM
Mukama na Ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni huyo na Ujumbe wake, mbele ya Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, kwenye jengo ilimozaliwa TANU.Picha na Bashir Nkromo