KESI YA JOHN TERRY YAENDELEA KUUNGURUMA MAHAKAMANI, MWENYEWE AKANUSHA MADAI YA UBAGUZI.
Posted on
Jul 10, 2012
|
No Comments
John Terry, mwenye umri wa miaka 31, na ambaye ni mchezaji soka wa Chelsea na vile vile timu ya taifa ya England, anashtakiwa kwa madai kwamba alimtukana Anton Ferdinand, kwa kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi katika mechi uwanjani, madai ambayo John Terry ameyakanusha.
Ikiwa John Terry atapatikana na hatia, hukumu kali zaidi itakuwa ni kutozwa faini ya pauni 2,500.
Kesi hiyo inatazamiwa itaendelea kwa siku tano katika mahakama yaWestminster, mjini London.
Inadaiwa kwamba mlinzi huyo waChelsea alimuita mwenzake mweusi, na akitumia maneno pia yaliyohusishwa na ngono.
Mtaalamu wa lugha ya kutafsiri yaliyosema kwa kuangalia mdomo, Susan Whitewood, alithibitisha kwamba matamshi yasiyofaa yalitumiwa na Terry.