MAHAKAMA KITENGO CHA BIASHARA SASA KUTUMIA SIO ZAIDI YA SIKU 462 KUTATUA MGOGORO WA KIBIASHARA.
Posted on
Jul 20, 2012
|
No Comments
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mawakili, wanasheria na wafanyabishara wakati wa kikao cha pamoja cha kujadili mbinu za kutekeleza kwa ufanisi na kwa njia fupi mashauri yanayowasilishwa katka mahakama hiyo.
Akizungumzia kikao hicho amesema kitu cha msingi katika mahakama hiyo kwenye kutatua migogoro ya kibiashara sasa kitakuwa kikichukua muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu kutatua mgogoro wa kibiashara uliowasilishwa mahakama kuu
Aidha katika maelezo yake ametolea mfano nchi nyingine duniani zikiongozwa na Singapore inayotumia siku 150, Rwanda siku 230 na kuwa kwa sasa Tanzania ni nchi ya 36 duniani katika kutatua migogoro ya kibiashara.
Ameongeza kusema kuwa sasa Tanzania imeamua kushughulikia suala hilo kiufanisi.