photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> MAKALA:TUSICHANGANYE SIASA NA MAISHA YA WATU.

MAKALA:TUSICHANGANYE SIASA NA MAISHA YA WATU.

Posted on Jul 14, 2012 | No Comments

Na Peter uiso
                Wakati Tanzania inatimiza miaka hamsini(50) tangu ipate uhuru na miaka ishirini(20)tangu iingie katika mfumo wa vyama vingi watanzania wengi wameanza kuuelewa mfumu huu kinyume na awali.
               Pindi mfumo huu ulipokuwa ukianzishwa watanzania walio wengi waliamini haukuwa mzuri na yawezekana walikuwa wakikaribisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
               Hata hivyo busara za hayati baba wa taifa zilitumika na kufanikiwa kuwabadilicha watanzania walio wachache na hatimaye baadaye watanzania waliowengi wakaingia katika mfumu wa vyama vingi.
             Hata ivyo mwalimu nyerere halisha wahi kuliasa taifa hili kuwa taifa bora lazima liwe na vitu vine ili liweze kuwa taifo bora lazima liwe na siasa safi,uongozi bora,watu na ardhi
             Hivi karibuni tumeshuhudia migomo mbalimbali ikiendelea nchini ikiwemo migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na na madaktari hapa nchini na hususani huu wa madakitari umekuwa ndio gumzo kwa watanzania walio wengi.
             Chakushangaza zaidi pamoja na madakitari kuwa na madai ya msingi ikiwemo kuboreshewa mazingira yao ya kazi vyama vya kisiasa vimekuwa vikitumia nafasi zao katika katika kuwapotosha watanzania kuwa mpaka sasa mgomo wa madaktari umekisha uku vyombo mbalimbali vikiwa vinatoa taarifa ya mgoma wa mdakitari kuendelea kushika kasi zaidi.
              Vyama vya kisiasa vimekuwa vikitumia nafasi zao bungeni  kujadili  hoja ya mgomo kama hoja ya dharura kutokana na kuwepo mahakamani wamekuwa wakiiwaacha watanzania kuendelea kufa pasipo hatua yoyote na kusubiri maamuzi ya upande wa maahakama kutoa uamuzi juu ya
la hili ambalo linaendelea kumaliza maisha ya watanzania walio wengi.
              Pamoja na hali hiyo bado kumekuwepo na vitendo vya wakukatisha tamaa madaktari na kuwafanya wao kuogopa kufuatili madai yao ya msingi ambayo wamekuwa wakiyafuatilia kama kipigo kikali kilichotokea  hivi karibuni cha kupigwa na kuumiza kwa mwenyekiti wa chama cha madaktari (Dr ulimboka) ambacho kiliwashtuwa madaktari wengi na  lakini walihahidi kutokata tamaa za kutafuta haki zao.
              Hata hivyo serikali haikushia hapo ilienda mbali zaidi kwa upande wa madaktari kwa kuwa simamisha kazi na madaktari wote ambao, waliogoma pamoja wakiwemo madaktari ambao walikuwa katika mafunzo kwa vitendo na madaktari bingwa pasipo kuangalia adhari zake kwa taifa ambalo lipo nyuma kimaendeleo hususani ya kijamii.
             Hivi ni kweli serikali ina lengo la kuwasaidia watanzania ,hasa wale wenye kipato cha chini  nashauri kuwa serikali lazima ielewe kuwa inawajibika kwa watanzania na vile vile watu huwajibika kwa serikali yao                                             
      0713-162905

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru