MAMA AFUNGWA JELA MIAKA 14 KWA JARIBIO LA KUMTOA KAFARA MWANAE.
Posted on
Jul 17, 2012
|
No Comments
Si kwamba ni mtoto wa kambo lah! Ni mwanae wa kumzaa mwenye umri wa miaka kumi, mama huyo aliamua kumtoa kafara mototo wake wa kiume ili apate shilingi million 80 za Uganda.
Mahakama kuu ya mjini kampala imememuhukumu mama huyo Joyce Barua, kifungo cha miaka 14 jela baada ya mama huyo kukiri kumsafirisha mwanae Innocent Edward Mani siku ya januari 27,2011 kutoka wilaya ya Isingiro kwenda Kisugu kwa mganga aitwaye Nyombi kwa lengo la kumtoa mtoto kafara.
Kwa baati nzuri police walipata taarifa kabla na hivyo kumtia mbaroni Joyce Barua kabla ya kumtoa kafara mwanae.