MATUKIO YA RAIS KIKWETE NA MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL ZANZIBAR KUFARIJI WALIOPATWA NA AJALI YA MELI
Posted on
Jul 19, 2012
|
No Comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu
huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali leo July 19, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo Julai 19, 2012 kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya Meli ya Skiget mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR




