photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MBUNGE AFANYA MAPENZI KWENYE GARI NA MWANAFUNZI..

MBUNGE AFANYA MAPENZI KWENYE GARI NA MWANAFUNZI..

Posted on Jul 21, 2012 | No Comments

Mbunge wa Misri wa chama cha Kiislamu chenye msimamo mkali, amekutikana na makosa ya kuvunja adabu ya kijamii, kuhusu tukio ambapo amekutikana anafanya mapenzi ndani ya gari lake.
Bunge la MIsri kabla ya kufungwa
Kesi hiyo imewatia aibu Waislamu wanaoitwa Salafi - ambao wanadai kuwa wanaume watengwe kabisa na wanawake.
Mbunge huyo, Ali Wanis, alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja na nusu, kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi, na kwa kumshambulia askari polisi.
Mbunge huyo ni wa chama cha Nour, kwenye bunge la mwanzo kuundwa baada ya utawala wa Rais Mubarak - bunge ambalo lilifutwa mwezi uliopita baada ya mahakama kuamua kuwa bunge hilo siyo halali.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru