photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MIILI 24 IMEPATIKANA HADI SASA, MATUKIO ZAIDI KATIKA PICHA KUZAMA KWA MELI IENDAYO ZANZIBAR

MIILI 24 IMEPATIKANA HADI SASA, MATUKIO ZAIDI KATIKA PICHA KUZAMA KWA MELI IENDAYO ZANZIBAR

Posted on Jul 18, 2012 | No Comments

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

-Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhiwaliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar.

Abiria waliyookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar.

Raia wa kigeni waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama  huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250
 Leo ni siku majonzi makubwa kutokana na ajali ya meli ya Star Gate iliyokuwa ikielekea Zanzibar. Tunaungana na Watanzania wengine kuwapa pole wahanga na wale waliopoteza ndugu na wapendwa wao katika ajali hiyo na kuwaomba wawe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru