MTALAKA WA RAIS ZUMA AULA KAMISHENI YA AU.
Posted on
Jul 16, 2012
|
No Comments
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Nkosazana Dlamini-Zuma amechaguliwa kuwa Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
Mwanamama huyo, mtalaka wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliibuka mshindi baada kumwangusha aliyekuwa akiishikilia nafasi hiyo, Jean Ping wa Gabon.
Akitangaza matokeo hayo juzi, Mwenyekiti wa AU, Rais wa Benin, Boni Yayi alisema kwa mara ya kwanza Afrika inapata kiongozi wa juu mwanamke, hivyo ni dhahiri kwamba mchango na uwezo wa wanawake unakubarika na kuaminiwa.
Rais Zuma ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumpongeza mtalaka wake na kumuelezea kuwa ni mwanamke jasiri na kwamba Afrika haitajuta kuwa na kiongozi wa aina yake.