photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > NDOA NDOANO; BOSS ANATAKA KUNITENGANISHA NA MKE WANGU

NDOA NDOANO; BOSS ANATAKA KUNITENGANISHA NA MKE WANGU

Posted on Jul 13, 2012 | No Comments

Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.

Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua


Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake
.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru