photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > NDOA NDOANO; MKE WA MTU ANANITAKA

NDOA NDOANO; MKE WA MTU ANANITAKA

Posted on Jul 9, 2012 | No Comments

Nina umri wa miaka 30 single... tangu nimeachana na girlfriend wangu miaka mitatu iliyopita imekuwa ikiniwia vigumu kuconnect with a woman, so nimekuwa na marafiki wa kawaida, kati ya marafiki hao, ni huyu dada. Ni age mate, mwaka wa nane yuko kwenye ndoa na ana watoto wawili sasa, urafiki ulianza wa kawaida tu, mara nyingi amekuwa akiniomba ushauri kuhusu mambo mbalimbali na mimi bila hiyana nimekuwa nikimpatia ushauri huo.... miezi sita iliyo pita aliuguliwa na mtoto wake, mimi kama rafiki nilitoa msaada mwangu kulingana mazingira yaliyokuwepo kwa huruma tu rafiki yangu anauguliwa... baada ya mtoto kupona balaa ndipo lilipoanzia, kwanza alianza na shukrani za kilio kwa kudai nilichomfanyia hajawahi kufanyiwa na mtu yeyote... halafu akaanza kunipa historia ya maisha yake ya ndoa, kwanza alilazimishwa kuolewa, na huyo mume wake kila siku ni vipigo, na akadai kuwa huyo mume wake mtoto wake wa pili si wake kwa sababu eti alishaenda kwa daktari akamwambia kuwa hana uwezo wa kuzaa tena... na huyo dada anadai hajawahi kutoka nje ya ndoa.. kwa hiyo umekuwa ni ugomvi mtindo mmoja, si kwa mawifi hadi kwa mama mkwe wake....Nilichokifanya ni kumpa tu ushauri wa kukaa na mumewe wayazungumze wayamalize na ikiwezekana wakafanye DNA ili kuondoa utata...kilichonishangaza akaanza kunambia she is deeply in love with me.. na muda mrefu amesubiri labda nitasema kitu sisemi amejaribu kila njia kunionyesha ila mimi nikawa kipofu... nilipomwambia kuwa siko tayari si tu kwa kuwa yeye ni mke wa mtu pekee bali bado kuna ghost linani haunt siko ready kuwa kwenye mahusiano kwa sasa bado aliendelea kung'ang'ania.... ananijua vizuri kila uongo nilioutumia kumkwepa ilikuwa ni kazi bure...
Najisikia vibaya sio kwamba ni mlokole, ila pia si mfuasi wa shetani, ninge hit nikakimbia lakini kila likinijia wazo la kuwa huyu ni mke wa mtu nashindwa, kibaya zaidi anasema yuko tayari ku sacrifice everything hata ikibidi kuivunja hiyo ndoa kwa ajili yangu... hicho ndio kinaniogopesha zaidi, kwanza najifeel guilty kwa kuiweka mashakani ndoa ya mtu pili hata nikikubali ipo siku yatanikumba kama ya huyo jamaa...TAFADHALI NAOMBA USHAURI WENU.... kama utanitumia email nitashukuru zaidi ...... ngomz25@gmail.com............. .THANX

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru