NDOA NDOANO; NIMWAMBIEJE?..
Posted on
Jul 22, 2012
|
2
Comments
Habari zenu wadau wa rchugga?Nilikuwa na boyfriend kwa miaka mitatu, tukaachana ktk hali ambayo iliniumiza sana moyo wangu, nikawachukia wanaume.Nikakaa kwa miaka miwili bila boyfriend. Sasa akatokea huyu kijana, akanipenda, kwa kuwa nilikuwa sitaki kuwa naye nikiogopa kuumizwa tena, nikamwambia nina mpenzi so aachane na mimi. Hakukata tamaa, akaendelea kunishawishi, hasa kwa kuwa tulikuwa tunaonana mara kwa mara - sehemu tunazofanyia kazi huwa tunaonana mara kwa mara na kwa kipindi cha kama miezi mitano nimekuwa nafanya naye kazi kwenye team moja ya consultancy.Nikajikuta naanza kumpenda, nikaanza naye uhusiano yeye akijua kuwa nina mpenzi na yeye ni kama anaiba tu. Sasa ndio nampenda mno na napenda niwe na mahusiano naye rasmi na serious. Sitaki kumpoteza. Tatizo ni je, namwambiaje kwamba nilimdanganya?Inakuwa vigumu kwangu kujua nianzaje kumwambia kwa sababu nilimjengea mazingira kuwa nina mpenzi serious, akawa haji au anaogopa kuja nyumbani kwangu; anajua hakika mwenyewe akirudi itakuwa balaa. Nilimdanganya BF wangu amehamia Mwanza na kwamba huwa naenda kumsalimia na yeye huja kwangu, nipo Dodoma kwa sasa. Ni kweli nilisafiri kwa private consultancy kwenda Mwanza mara mbili, na huyu boyfriend mpya aliamini kuwa naenda kwa mpenzi. Mimi huwa naenda nyumbani kwa huyu BF mpya bila tatizo lolote, na sasa baadhi ya watu wake wa karibu wameshanifahamu.Naomba ushari wenu, ipi ni namna nzuri ya kurekebisha makosa niliyofanya? Natanguliza shukrani.
Share your story here, email us rchugga@gmail.com
pole sana dada kwa jutokuwa mkweli kwake, cha msingi mi naona usimwambie kuwa ulikuwa unamdanganya bt jifanye umeachana na yule mpenzi wa kwanza kabisa nass upo tiyari kuwa huru na huyu BF mpya, sababu wanaume wengi wakigundua uliamdanganya hata kama kwa nia njema ujue graph yako ya mapenzi ndo inashushwa kabisa na mwanaume hata badilika kamwe kukukubali. yangu ndiyo hayo mwl. c.nadila.
ReplyDeletepole sana dada kwa jutokuwa mkweli kwake, cha msingi mi naona usimwambie kuwa ulikuwa unamdanganya bt jifanye umeachana na yule mpenzi wa kwanza kabisa nass upo tiyari kuwa huru na huyu BF mpya, sababu wanaume wengi wakigundua uliamdanganya hata kama kwa nia njema ujue graph yako ya mapenzi ndo inashushwa kabisa na mwanaume hata badilika kamwe kukukubali. yangu ndiyo hayo mwl. c.nadila.
ReplyDelete