photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > NDOA NDOANO; WAZAZI WAKE WANAGOMA NIFANYEJE??

NDOA NDOANO; WAZAZI WAKE WANAGOMA NIFANYEJE??

Posted on Jul 10, 2012 | 1 Comment

Nimekuwa na mahusiano na huyu binti kwa miaka 2 sasa nafsi yangu imeridhika naye na tulipanga baada ya yeye kumaliza masomo tuanze mipango ya ndoa, sasa kamaliza masomo yake....aliwaeleza wazazi wake kuhusu mimi na kwamba tunaitaji kupeleka posa kabla ya mipango mingine ya harusi cha kushangaza baba yake aligoma kwamba binti yake ni mdogo (22yrs) kiukweli sina amani coz tunaishi mikoa tofauti na hata kuonana inakuwa kazi sasa kwa sababu yuko home kwao ni ngumu sana kutoka naona kama naweza mkosa kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu. Yeye yuko tayari na ameridhia tatizo ni mzazi wake na ndiye anapaswa kumsikiliza, imefikia hatua nafikiria kumpa mimba ila kwa upande mwingine naona si sahihi. Naomba msaada wenu wa kimawazo kwa sababu hili swala linaitaji ridhaa ya wazazi ili kujenga uhusiano bora na familia yao

Comments:1

  1. Nataka kujua, hayo masomo alomaliza ni ya Degree au ni High school tu?

    Kama ni high school yaeza kua kweli ndo maana baba yake anakataa. Hakuna mzazi anaekataa bint ake acolewe bila sbb. Unajua sa hv akiolewa masomo yatacmama kwa mda.

    Pia wewe una umri gan? Na je unaona yeye anaeza kucmamisha familia kwa umri aloanao?

    Pia hilo jiulize. Othrwise kua tu mvumilivu aana ucmpe mimba kwa sbb ya kukataliwa wengi wamefanya makosa na kutamani wacngefanya hvy.

    Kila la heri. Kidodii

    ReplyDelete