photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KATIKA SEHEMU ZA HISTORIA ZANZIBAR

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KATIKA SEHEMU ZA HISTORIA ZANZIBAR

Posted on Jul 18, 2012 | No Comments

 Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali akiwanesha waandishi Ramani ya Mji wa Zanzibar ulivyokuwa kabla na kubainisha mabadiliko mbalimbali yaliotokea.
 Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali walifika huko maruhubi na kupata historia ya majengo hayo ambaya yalijengwa na Mfalme Baraghash kwa ajili ya Starehe tu katika mwaka 1880 na kuharibika kwa kuungua moto mwaka 1889.
 Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali walifika huko Mangapwani na kupata historia ya Kisima cha chini kwa chini kwa Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali.
 Waandishi wa Habari wakiwa Ndani ya Kisima cha Chini kwa chini chenye Urefu wa zaidi ya Kilomita moja katika kila pembe ya ndani ya kisima hicho.
 
 Hii ni nyumba ya chini kwa chini iliojengwa na Waarabu kwa ajili ya maficho ya Watumwa baada ya kupigwa marufuku Biashara hio mwaka 1873 huko katika kijiji cha Mangapwani kaskazini Unguja.
Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali akiwaongoza Waandishi kuingia ndani ya Nyumba ya chini kwa chini iliojengwa na Waarabu kwa ajili ya maficho ya Watumwa baada ya kupigwa marufuku Biashara hio mwaka 1873 huko katika kijiji cha Mangapwani kaskazini Unguja.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru