photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > BOMU LA MKOLONI LAKUTWA BABATI LIKIWA ZIMA.

BOMU LA MKOLONI LAKUTWA BABATI LIKIWA ZIMA.

Posted on Aug 17, 2012 | No Comments

Kamishna msaidizi Akili Mpwapwa
Na Mwandishi wetu; Bilhuda Msangi 
Manyara:
Bomu lililoachwa miaka iliyopita lililokuwa linatumiwa na askari wa zamani wa uingereza (KAR)
limepatikana kwenye kijiji cha Endanoga,kata ya Galapo wilaya ya Babati mkoani Manyara likiwa bado lizima.

Akidhibitisha kupatikana kwa bomu hilo,Kamanda wa polisi Mkoani  Manyara kamishna msaidizi Akili Mpwapwa
amesema limepatikana kwenye shamba la Barie Ibrahim mkazi wa kijiji hicho cha Endanoga

Amesema Ibrahim alikuta bomu hilo majira ya mchana likiwa zima na lenye uwezo wa kutumika wakati akichimba
udongo wa kufyetulia matofali katika shamba lake kwenye kijiji hicho ndipo akatoa taarifa kwa uongozi wa kijiji cha Endanoga.

Amesema askari polisi kwa kushirikiana na askari wa jeshi la kujenga taifa JWTZ pamoja na wataalamu wa kulipua mabomu
 walifanikiwa kulitegua bomu hilo ambali lilikuwa lizima japokuwa halikutumika kwa muda mrefu na halikuleta madhara
kwa mtu yoyote.

Amesema polisi wakishirikiana na wataalamu wa kulipua mabomu kutoka JWTZ wanaendelea na uchunguzi ili kubaini
 kama kuna mabomu mengine yameachwa na askari hao ili wananchi wasipate madhara.

Kamanda Mpwapwa ameongeza kuwa bomu hilo lilikuwa linatumika na askari wa zamani wa Uingereza (KAR)
waliokuwa wanawafundisha askari wa kitanzania mara baada ya kupatikana kwa uhuru wa nchi mwaka 1961.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru