photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > BREIVIK MTUHUMIWA WA MAUAJI NORWAY AHUKUMIWA MIAKA 21 JELA..

BREIVIK MTUHUMIWA WA MAUAJI NORWAY AHUKUMIWA MIAKA 21 JELA..

Posted on Aug 24, 2012 | No Comments

Breivik anatabasamu
Mahakama ya Norway imeamua kuwa Anders Behring Breivik ana akili zake timamu, na imemhukumu kifungo cha miaka 21 kwa kuuwa watu 77 mwezi wa Julai mwaka jana.
Breivik siku zote amekiri kufanya mashambulio ya mabomu na bunduki, bila ya kuonesha majuto.Upande wa mashtaka ukitaka kupata uamuzi juu ya akili ya Breivik, na angekutikana punguani angewekwa kwenye jela ya wendawazimu kwa muda usiojulikana.
Amekuwa akishikilia kuwa ana akili yake, na kwamba aliyofanya ni vitendo vya kisiasa.
Alitabasamu hukumu ilipotolewa.
Wakili wa Breivik amethibitisha kuwa mteja wake hataomba rufaa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru