photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > CLOUDS MEDIA GROUP YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA AMANI CENTER

CLOUDS MEDIA GROUP YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA AMANI CENTER

Posted on Aug 25, 2012 | No Comments

            Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh Dr Msengi akikabidhi sehemu ya msaada kwa muwakilishi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira cha Amani Center kilichopo nje ya mji wa Moshi,kwa mratibu wa kazi za kijamii Japhary Salum,Msaada huo umetolewa jioni ya leo na kampuni ya Clouds Media Group,ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuisaidia jamii.
Pichani anaezungumza nia Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini,Mh Dr Msengi akizungumza kwa ufupi ikiwemo sambamba na kuishukuru kampuni ya Clouds Media Group iliombatana na baadhi ya wasanii,kwa namna ambavyo wamekuwa wakiijali jamii kwa namna moja ama nyingine,shoto ni Mratibu wa shughuli hiyo kutoka Clouds,Simon Simalenga na mwisho shoto ni mratibu wa kazi za kijamii Japhary Salum pamoja na Afisa Ustawi wa jamii wa Moshi,Bwa. Sammy Mulemba.
Mratibu wa shughuli hiyo kutoka Clouds,Simon Simalenga akimkaribisha Mkuu wa Wilaya na wageni wengine waalikwa mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,kwenye moja ya darasa la kituo hicho cha Amani Center.
OfisaMawasiliano wa kituo cha Amani Center,Salima  Khatibu akitoa maelezo na historia fupi ya kituo hicho kwa baadhi ya wasanii walioshirikiana na kampuni ya Clouds Media Group kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho jioni ya jana.
OfisaMawasiliano wa kituo cha Amani Center,Salima  Khatibu akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Moshi mjini,Mh.Dr Msengi alipowasili kwenye kituo hicho kwa niaba ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula.

Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kushirikiana na kampuni ya Clouds Media Group kutoa msaada huo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru