photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > HISTORIA FUPI YA ALIYEKUWA RAIS WA ETHIOPIA, MELES ZENAWI..

HISTORIA FUPI YA ALIYEKUWA RAIS WA ETHIOPIA, MELES ZENAWI..

Posted on Aug 21, 2012 | 1 Comment

Meles Zenawi afariki

Alikuwa na umri wa miaka hamsini na saba na ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa na ambaye utawala wake ulikumbwa na utata barani afrika.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa sasa ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitali, ''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki jana mwendo wa 23:40,'' taarifa hiyo imesema.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga ameiambia BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi.
Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama kiongozi mashuhuri na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la afrika.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa kuchukua mahala pake.

Comments:1