photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MAFURIKO YASABABISHA VIFO NIGERIA

MAFURIKO YASABABISHA VIFO NIGERIA

Posted on Aug 15, 2012 | No Comments

Mafuriko katika eneo la Jos
Mafuriko katika eneo la Jos
Takriban watu 33 wameuawa kufuatia mafuriko makubwa kati kati mwa jimbo la Plateau nchini Nigeria.
Afisa mmoja wa shirika la kutoa misaada, Abdussalam Muhammad ameiambia BBC, kuwa maelfu ya watu wameachwa bila makao baada ya makaazi yao kusombwa na maji.
Amesema usafiri umetatizika baada ya barabara kadhaa na daraja kusombwa na maji na hivyo kuvuruga shughuli za kutoa misaaada.
Zaidi ya watu elfu kumi na mbili wameathiriwa na mafuriko hayo yaliyokumba wilaya sita ikiwemo wilaya ya Shendam.
Mwezi uliopita watu thelathini na tisa waliuawa karibu na makao makuu ya jimbo hilo Jos.
Maafisa wa serikali wamewaonya raia katika maeneo hayo kuwa huenda kukatokea mafuriko zaidi katika siku za hivi karibuni.
Msimu wa mvua nchini Nigeria huanza mwezi Machi hadi Septemba Kila mwaka.
Bwana Muhammad, ambaye ni mshirikishi wa kutoa misaada ya dharurua wa shirika la kitaifa la kukabiliana na majanga katika eneo la kati nchini Nigeria, amesema waathiriwa hao wanahitaji misaada ya vyakula, maji, mavazi, blanketi na dawa.
Wilaya ya Shendam ni miongoni mwa sehemu zilizoathiriwa pakubwa na mafuriko nchini Nigeria.
Sehemu zingine ni pamoja na wilaya za Wase na Kanam.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru