photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > REDDS MISS MWANZA 2012/13 KUFANYIKA AGOSTI 31

REDDS MISS MWANZA 2012/13 KUFANYIKA AGOSTI 31

Posted on Aug 1, 2012 | No Comments

Mrembo wa mkoa wa Mwanza 2012/13 atapatikana ijumaa ya agosti 31 katika viwanja vya Yatch Club Mwanza.
 
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na muaandaji wa kampuni ya Sisi Entertainment
John Doto, amesema shindano hilo linalovuta hisia za wengi ndani ya mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla,
litashirikisha warembo tariban 20 kutoka wilaya zote za mkoa Mwanza.
John
Doto amesema warembo wote watakaa kambini kwa wiki mbili, ambapo kambi rasmi itaanza tarehe 20 agosti mwaka huu katika hoteli ya Isamilo Lodge.
Shindano la Redds Miss Mwanza 2012/13, lilisogezwa mbele kufuatia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wakiwa
kambini warembo watapata fursa ya kujifunza Mitembeo, Tabasamu, ufahamu wa kujieleza pamoja na kuvumbua vipaji mbalimbali.
John
Dotto pia amesema warembo watakua na ziara ya kwenda kwenye mbuga za wanyama Serengeti, kutoa misaada kwa watoto yatima, vikongwe pamoja na kufanya usafi kwenye moja ya Hospitali Jijini Mwanza na moja ya barabara za Mwanza.
Kwa
miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Mwanza umekua ukitoa warembo wanaofanya vizuri

mashindano ya Taifa.
Itakumbukwa

Mwaka 2008 Nasreem Karim na Mwaka 2009 Miriam Gerald waliweza kushika Mataji ya
Miss Tanzania wakitokea mkoa Mwanza.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru