SAKATA LA CHRIS BROW NA DRAKE KATIKA KLABU YA USIKU HUENDA LIKAWAGHARIMU HADI DOLA MILION 16.
Posted on
Aug 16, 2012
|
No Comments
Sakata la kurushiana chupa lililoanzishwa na wasanii maarufu nchini Marekani Chris Brown na Drake katika klabu moja ya usiku huenda likawagharimu hadi dola milioni 16.
Kwa mujibu ya NewYorkPost tuhuma zimefunguliwa dhidi yao katika mahakama kuu ya jimbo la Manhattan, ambapo kampuni ya Entertainment Enterprises Ltd inadai kuwa mastaa hao ndio walianzisha vurugu pacha za Greenhouse na WiP mnamo tarehe 14 mwezi Juni na kuwaamuru wapambe na mashabiki wao kuingilia.
Mashitaka yaliyofunguliwa yanata kushikiliwa kwa Brown na Drake, ambao hakuna kati yao aliyefunguliwa mashitaka ya uhalifu, kuhusiana na sakata hilo.
Faili hilo lililofunguliwa linamadai ya dola milioni 16 kama hasara kutokana na uzembe wa wasanii hao na kufanya vitendo vya hatari na kwa makusudi kufanya vitendo kinyume na sheria.