photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > SIFA 12 ZA MWANAUME WA KWELI (A REAL MAN) TENA WA KIAFRIKA

SIFA 12 ZA MWANAUME WA KWELI (A REAL MAN) TENA WA KIAFRIKA

Posted on Aug 17, 2012 | No Comments


Ndugu wadau, baada ya kuona na kushiriki mijadala mingi, nimeonelea nitoe mchango wangu ili ndugu, dada, binti na wajukuu zetu waweze kuelewa tunavyomfahamu mwanamume wa kweli (A real man) tena wa Kiafrika.
1.Siku zote hujitahidi kwa kila njia kuonesha kuwa yeye ni mwanamume na siyo mvulana mkubwa (big boy) au mwanamke asiye kuwa na maziwa huku akiwa ndani ya suruali.
2.Hufanya maamuzi pale pale inapotakiwa na husimama kidete kuhakikisha maamuzi yake muhimu (yale ya busara) yanatekelezwa tena kwa gharama yoyote. Mwanamume wa kweli hatoi kauli tata na kauli zake huwa ni aina fulani ya maelekezi (orders) ya jinsi ya kudeal na issues zote muhimu ndani nyumba!
3.Huwa halii lii ovyo hata kama kafiwa. Hujitahidi kutowaambukiza weliomzunguka emotional break down. Kwa hiyo, inapobidi kulia, huficha sura yake. Mwanamume wa kweli hawezi kuangua kilio mbele za watu hata kama kafiwa na Mungu wake!!
4.Hatelekezi familia hata siku moja bali uhakikisha ustawi wa familia yake unakuwa kipaumbele chake cha kwanza. Watoto watapata matunzo mazuri (bila ubaguzi) kwa kadri ya uwezo wa familia na mke wake atapewa kipaumbele cha kwanza katika matumizi ya rasrimali za familia (family resources)
5.Hufanya kila njia mke wake awe na furaha na amani kwa kumpa haki zake zote za ndoa bila mzaha (she needs a full dose).
6.Inapotokea akachepuka mara moja moja, hutengeneza mikakati ya kuhakikisha kuwa tahadhari kubwa imefanyika ili kumlinda mke wake na familia kwa ujumla…Ushauri wa The Boss hutumika katika mambo haya.
7.Husimama kwenye mstari ili kusimamia mambo ya msingi (principles) katika uendeshaji wa familia yake kama kiongozi imara. Na pale anapokosea, hutumia mbinu za kiutu uzima kuweka mambo sawa. Kamwe hatakubali shinikizo la mke wake katika kutatua matatizo ya kifamilia ndani ya nyumba yake!
8.Mwanamume wa kweli hafanyi mambo ya mzaha mzaha na kuomba omba misamaha isiyo na kichwa wala miguu! Hata hivyo, anaweza kuomba msamaha kwa mke wake katika mambo ambayo hayagusi misingi na uwepo wa ndoa. Ila kamwe, hatakiwi kukiri kutoka nje ndoa. Hata pale anapokamatwa ugoni (labda akutwe bolt imefungwa na nut), atatumia mbinu zozote ikiwa ni pamoja na msaada wa wanaume wenzake (wakati mwingine hata wanawake) kutunza imani ya mke kwake. Hata siku moja, hatakiwi kumweleza mke wake (kwa kinywa chake) eti katembea nje ya ndoa.
9.Siku zote atakuwa mwanamume na baba na hatafanya michezo ya kucheka cheka kipuuzi ama mbele ya watu au wanafamilia…Lazima kila kinywa kikiri kuwa kweli huyu ni baba ndani ya nyumba!!
10.Hakimbii matatizo hata yakiwa makubwa kiasi gani…Atayakabili kwa mbinu zozote zile ili kulinda heshima ya uanaume na ubaba wake….Ndiyo maana, watoto wadogo wanaamini kuwa baba hashindwi na jambo lolote. Kuwaonesha watoto na hata mke kuwa baba ana vitu asivyoviweza ni kuwaharibu kisaikolojia!
11.Ataonesha siku zote kwamba hasemi uongo. Hata pale atakaposema uongo mtakatifu (mfano, kumficha kitu mke wake ili kutomvunja moyo au kuharibu imani yake kwake), atalinda maneno yake kwa gharama zozote!!
12.Atapigania himaya yake kwa nguvu na gharama zozote zile….Hawezi kukubali kudhalilishwa mbele ya mke na watoto wake! Bora afe kuliko kuona hayo yakifanyika machoni pake!

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru