photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > TANZANIA KUWA MWENYEJI JUKWAA LA MAPINDUZI YA KIJANI AFRIKA MWEZI SEPTEMBA 2012

TANZANIA KUWA MWENYEJI JUKWAA LA MAPINDUZI YA KIJANI AFRIKA MWEZI SEPTEMBA 2012

Posted on Aug 23, 2012 | No Comments

 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mh. Christopher Chiza (katikati) akizungumzia jukwaa la mapinduzi ya kijani Afrika litakalokutanisha viongozi mbalimbali ambapo amesema Tanzania inawakaribisha viongozi kutoka pande zote za dunia kujadili na kutafuta njia mpya ya kuongeza mafanikio katika kilimo ili kuweza kujiimarisha zaidi katika suala zima la kilimo. Kulia ni Rais wa AGRA Bi. Jane Karuku na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Muhammed Muya.
  Rais wa AGRA Bi. Jane Karuku akizungumza ambapo amesema jukwaa litaendelea kujadili na kutafuta njia bora za kuboresha kilimo barani Afrika. kushoto ni Mh. Chizza.

Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani (AGRF) limeandaa kongamano kwa viongozi wa Afrika  na kuendesha mpangilio wa kukuza uwekezaji na sera ya kuongeza uzalishaji wa kilimo na ukuaji wa kipato kwa wakulima wa Afrika.
Wakati wa kongamano hilo litakalofanyika mjini Arusha kuanzia tarehe 26 hadi 28 mwezi ujao mwaka huu, viongozi hao watapata fursa ya kujadili sera ya mapinduzi ya kilimo na uchumi wa Afrika, Njia za kukuza masoko na kujadili kwa pamoja katika kubadilisha mfumo mzima wa kilimo.
Jukwaa hilo litatoa fursa ya kujadili namna bora ya kuendeleza mipango ya uwekezaji wenye tija na kuongeza maendeleo ya kilimo barani ya Afrika.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru