WATANZANIA 27 WAHUSISHWA NA DOLA 186MILLION BANK ZA USWIZI
Posted on
Aug 19, 2012
|
No Comments
Watanzania 27 wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara ndio wamebainika kumiliki mabilioni ya fedha nchini Uswisi huku mmoja wao akimiliki Dola za kimarekani 56 milioni sawa na sh 89.6 bilioni za kitanzania.Kiasi cha fedha kinachomilikiwa na watanzania hao ni Dola za kimarekani 186 milioni ambapo ni sawa na zaidi ya sh 300 bilioni za kitanzania.
Taarifa zinasema kigogo mmoja anamiliki sh 90 bilioni na wengine wanne ni kama ifuatavyo.Mmoja dola 30 milioni(sh 48 bilioni),mwingine Dola 20 milioni( sh 32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni ambazo ni sawa na sh 16 bilioni.
Katika orodha hiyo wamo pia wafanyabiashara wanaomiliki kati ya Dola miloni 2 mpaka Dola milioni 7,kadhalika wamo waliowahi kuwa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza ambapo akaunti zao zina kiasi kisichozidi Dola 500,000 kila mmoja.
Taarifa zaidi zinasema fedha hizo ziliwekwa kwenye account za vigogo hao kwa mara ya mwisho mwaka 2005.

Tafakari....