photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > HUYU NDIYE MISS ILALA 2012 KWA WALE AMBAO HAMKUMWONA

HUYU NDIYE MISS ILALA 2012 KWA WALE AMBAO HAMKUMWONA

Posted on Sep 8, 2012 | No Comments

 
Na Mwandishi Wetu
Mrembo Noela Michael (18) usiku wa kuamkia jana aliibuka mshindi taji la Redds Miss Ilala 2012 katika shindano iliyofanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Noela ambaye anashikilia taji la Miss Tabata 2012 ambalo lilimpa tiketi ya kushiriki Miss Ilala mwaka huu. 
Mrembo Noela ambaye anajiandaa kuingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza kidato cha sita, aling’ara katika usiku huo ambao alipata upinzani mkali kutoka kwa Magdalena Roy Munisi (21) wa Dar City Centre aliyeshika nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mary Chizi wa Ukonga.
Kwa kutwaa umalika huo Noela amejishindia Sh. Milioni 1.5 wakati Magdelena amepata Sh Milioni 1.2 na mshindi wa tatu, Mary amepata Sh. 700,000.
Warembo wote watatu wataiwakilisha  kanda ya Ilala katika shindano la Redds Miss Tanzania litakalofanyika baadae mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru