Na Mwandishi Bilhuda Msangi.
Zoezi la kufukua Maiti za watu waliofunikwa na kifusi katika Machimbo ya Madini katika Kata ya Nandagala Wilayani
Ruangwa Mkoani Lindi jana limekamilika leo asubuhi huku wakifanikiwa kuzipata maiti zote 7
Diwani wa Kata hiyo, Andrew chikongwe alibainisha kuwa kazi ya kufukua kifusi hicho imechukua muda mrefu kufuatia kuwepo kwa zana duni za kufukua mchanga hali iliyofanya kazi hiyo kuwa ngumu kuanzia jana saa 9 jioni hadi leo asubuhi
Chikongwe aliwataja Marehemu hao ni Nyang'ana Mkelecha,Mkazi wa Musoma,Mohamed Omari Fondogoro,Mkazi wa Morogoro,Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa,Rajab maarufu ROGER Mkazi wa Musoma,Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo,Chakoda Mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu BADE Mkazi wa Masasi mkoani Mtwara.