RAIS KIKWETE AWASILI KAMPALA KUHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU
Posted on
Sep 8, 2012
|
No Comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Septemba 7, 2012. Rais Kikwete amewasili nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. Kalonzo Musyoka aliyemtembelea katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Septemba 7, 2012 ambako wote wamewasili kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. Kalonzo Musyoka aliyemtembelea katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Septemba 7, 2012 ambako wote wamewasili kuhudhuria mkutano wa siku moja wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.(Picha na IKULU).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda baada ya mazungumzo mafupi katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala leo Septemba 7, 2012. Rais Kikwete amewasili nchini Uganda leo kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.