photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > AIR TANZANIA YAANZA TENA SAFARI ZAKE OKTOBA 12.

AIR TANZANIA YAANZA TENA SAFARI ZAKE OKTOBA 12.

Posted on Oct 10, 2012 | No Comments

Inaonekana Air Tanzania inafufuka taratibu. Jana kwenye facebook page ya kampuni, wametoa taarifa ya kuanza safari mbalimbali hapa nchini wiki hii, na wana mipango ya kuanza safari za nje miezi michache inayokuja. Taarifa ya ATCL kutoka facebook inasema:
” Tunapenda kuwataarifu kuwa kuanzia Ijumaa, 12 Oktoba 2012, tunarejesha upya huduma zetu za safari ambazo zilisitishwa kwa muda kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Tunaanza tena safari kati ya Dar es Salaam, Mwanza, na Kilimanjaro siku hiyo, na kupanua wigo wa huduma zetu katika miezi ijayo. Tunatarajia kuanza safari kuelekea Arusha na Zanzibar mwanzoni wa mwezi Novemba, na safari za Mtwara na Moroni Hahaya baadaye mwezi huo. Tunatarajia kusambaza huduma za safari hadi Dubai kabla ya mwisho wa mwaka.
Tunawashukuru sana nyote kwa uvumilivu wenu na kwa kuendelea kutuunga mkono.
Tafadhali tembelea ofisi zetu au za wakala wa usafiri kufanya booking kwa ajili ya kusafiri na Air Tanzania, The Wings of Kilimanjaro.”
air tanzania atcl Air Tanzania yarudi kwa nguvu

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru